HomeHabariMawakili wa Balozi Mstaafu, Humphrey Polepole wamezitaka mamlaka za usalama wa raia...

Mawakili wa Balozi Mstaafu, Humphrey Polepole wamezitaka mamlaka za usalama wa raia na mali zao

- Advertisement -spot_img

Mawakili wa Balozi Mstaafu, Humphrey Polepole wamezitaka mamlaka za usalama wa raia na mali zao kutumia mbinu na rasilimali zote za umma kuhakikisha, na kisha kutoa taarifa kwa umma wa Watanzania, na Dunia kwa ujumla, juu ya hali ya usalama, na maslahi ya kisheria ya Polepole.

Kupitia barua ya leo Oktoba 06, 2025 iliyoandikwa na Wakili wa Polepole, Adv. Peter Kibatala kwenda kwa Mamlaka husika, Mawakili hao wamezitaka Mamlaka husika kuhakikisha Polepole anapatikana akiwa hai na kubainisha kuwa watatoa taarifa zaidi kuhusu hatua watakazozichukua kwa kushirikiana na watu, na Taasisi mbalimbali Duniani kote.

Haya yanajiri ikiwa ni masaa kadhaa baada ya kusambaa kwa taarifa kutoka kwa baadhi ya ndugu wa Polepole wakidai kuwa Balozi huyo Mstaafu ambaye pia amehudumia Nchi yake katika nyadhifa mbalimbali za utumishi wa umma ametekwa huku Jeshi la Polisi likisema limeanza kufanyia kazi taarifa hizo ili kubaini ukweli wake.

polepole #robymedia #robynews
- Advertisement -spot_img
- Advertisement -spot_img
Stay Connected
16,985FansLike
2,458FollowersFollow
61,453SubscribersSubscribe
Must Read
- Advertisement -spot_img
Related News
- Advertisement -spot_img

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here