Home Uncategorized SIMBA DAY

SIMBA DAY

34
0

“Hakikisheni kwamba kama tawi, mnahusiana, mnashirikiana na kushiriki kikamilifu katika kila tukio linaloandaliwa na Klabu ya Simba. Klabu ya Simba ni taasisi kubwa yenye historia, heshima na mafanikio makubwa ndani na nje ya uwanja. Simba haina baya, bali kila siku inaleta mambo mapya yenye mvuto, mafanikio na matukio ya kupendeza kwa wanachama na mashabiki wake. Kwa sababu hiyo, ni wajibu wetu sote kujitayarisha mapema na kuhakikisha tunashiriki bila kukosa katika matukio hayo.Wiki hii, siku ya Jumatano, tutakuwa na tukio kubwa, la kihistoria na lenye kusisimua sana — ‘Simba Day’. Hii ni siku ya heshima, mshikamano na kusherehekea klabu yetu. Ni wakati wa kila mwanachama na shabiki wa Simba kuonyesha mapenzi ya kweli kwa klabu yetu kwa kushiriki kwa wingi, kwa mshikamano na kwa furaha kubwa.Nawahimiza wanachama wote wa Tawi la VIP A Magomeni kujipanga mapema, kuhakikisha wanahamasisha wengine, kuja kwa wingi na kushirikiana bega kwa bega. Hii ni nafasi ya kuonyesha mshikikano, mshikamano na uzalendo wetu kwa Simba SC. Tukutane uwanjani katika siku hii muhimu kwa kishindo na tukioneshe kwa vitendo nguvu ya upendo wetu kwa Simba.”— Kaimu Mkurugenzi wa Wanachama, Hamisi Kissiwa, akiongea na Wanasimba wa Tawi la VIP A Magomeni.

#za robymedia#T20 CLASSICInstagram: @official_arnold.1

ROBY MEDIA tunakuletea kilicho bora zaidi

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here